Mtanzania
ambaye hajatajwa jina amekamatwa na dawa za kulevya aina ya cocaine
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo nchini Msumbiji.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Orlando Madumane, Mtanzania huyo amekamatwa baada ya kutua uwanjani hapo akitokea Brazil.
Alikutwa
akiwa na jumla ya vidonge 70 vya cocaine kwenye tumbo. Kwa sasa
anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Maputo akisubiri kufikishwa
mahakamani.
No comments:
Post a Comment