Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Itobo katika Jimbo la Bukene na kuwaambia waimarishe mahusiano na viongozi wao ikiwa pamoja na kuwaamini katika utekelezaji wa shughuli za kila siku.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Itobo kwenye
viwanja vya Itobo Sokoni na kuwahakikishia wananchi wa Itobo kuwa CCM
inazidi kuimarika kila siku kwa sababu ndio chama pekee kinacho ongelea
matatizo ya wananchi na kuja na majibu ya matatizo hayo.
Mbunge wa Jimbo
la Bukene Ndugu Sulemani Zedi akihutubia wananchi kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Itobo Sokoni ambapo aliwaambia
wananchi hao miradi ya maji mitano ipo kwenye hatua za mwisho hivyo
tatizo la maji litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa.
Diwani wa Kata
ya Itobo Ndugu Amina Shija akihutubia wakazi wa Itobo na kuwaambia CCM
Imejipanga vizuri na itaendelea kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe wa uzinduzi wa mradi wa
kufyatua matofali wa UWT wilaya ya Nzega unaodhaminiwa na mbunge wa viti
Maalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa juu ya tanki la maji ambalo ni moja kati ya miradi ya maji ya Itobo.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji katika
kituo cha Uchama kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya maji Safi na Taka mjini
Nzega Ndugu Samuel Duyigi.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mkulima wa mpunga Ndugu
Mohamed Kashinde kuangalia namna mkulima huyo anaendesha kilimo chake
cha umwagiliaji,Itobo wilayani Nzega mkoa wa Tabora.
No comments:
Post a Comment