Pages

Thursday, May 1, 2014

RAIS KIKWETE KUWA MGENI RASMI SIKU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI LEO

RAIS Jakaya Kikwete (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia katika sherehe za wafanyakazi, Mei Mosi zitakazofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Hezron Kaaya mapema wiki hii aliwaambia wanahabari kuwa maadhimisho ya Sikukuu ya Mei Mosi mwaka huu yatafanyika kitaifa katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.
“Katika kikao chetu na Rais Kikwete alishangaa  kuona kuna mambo bado yamelala licha ya kuwa yameshafanyiwa kazi. Kuna suala la ukokotoaji kwa mifuko yote ya jamii kutofanyiwa kazi licha ya kuwa tayari wamefanya tathmini, lakini bado linasuasua,” alisema.
Alisema Rais pia alishangaa kwamba suala la kodi linaendelea kuwalemea wafanyakazi wachache walioko katika sekta rasmi na kuacha wengine wakiwa hawalipi kodi kwani nguvukazi ya nchi ni zaidi ya watu milioni 21, lakini wanaotozwa kodi ni milioni tatu pekee.
Aliongeza kuwa leo kutakuwa na maandamano ya wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali nchini ambayo yataanzia Mnazi Mmoja na kuishia katika uwanja huo wa Uhuru yatapokelewa na Rais Kikwete ambaye atazungumza na wafanyakazi hao.

No comments:

Post a Comment