Hatimaye beki wa kulia wa Arsenal, Bacary Sagna amekamilisha usajili wake Manchester City kwa kupewa mkataba wa miaka mitatu.
Sagna
amemaliza mkataba wake Arsenal, ambapo wakuu wa Emirates walikuwa
wakivuta miguu kumpatia mkataba mpya kwa sababu ya umri wake.
Sagna
(31) alikuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio Arsenal msimu uliomalizika
majuzi lakini Arsenal waliona kwamba umri na fedha alizokuwa akidai
vilikuwa juu.
Inaelezwa
kwamba awali alipewa mkataba wa mwaka mmoja Arsenal akakataa, akapewa
wa miaka miwili lakini wakashindwana kwenye malipo, akaamua kuondoka.
Alicheza
mechi yake ya mwisho kwenye fainali ya Kombe la Ligi wikiendi iliyopita
ambapo Arsenal waliibuka na taji baada ya miaka tisa.
Inaelezwa
kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamempa mkataba ambao
atalipwa pauni 150,000 kwa wiki, ikiwa ni nyongeza kubwa kutoka pauni
80,000 alizokuwa akilipwa Arsenal.
Hata
hivyo, Sagna ambaye kocha Arsene Wenger alijaribu kumbakiza, alikuwa
akitaka nyongeza hadi pauni 200,000 na miaka mitatu zaidi hapo Emirates,
kiwango ambacho kikilinganishwa na umri wake waliona hakikidhi
mahitaji.
Sagna
alikuwa pia akitakiwa kusajiliwa na klabu nyingine kubwa Ulaya kama
Paris Saint Germain, na Monaco za Ufaransa na Galatasaray ya Uturuki.
Kutokana
na mazingira hayo, Arsenal wameshaanza mazungumzo kwa ajili ya
kumsajili Serge Aurier anayecheza Toulouse ya Ufaransa kuziba nafasi ya
Sagna.
Aurier
anayethaminishwa kwa pauni milioni saba amesema wazi kwamba hawezi
kukataa ofa kutoka klabu yoyote ya Ligi Kuu England, hata zilizopanda
daraja msimu huu kwa sababu ni ligi kubwa.
Arsenal
wameshaanza mazungumzo na klabu yake, ambapo watalazimika kutoa fungu
huku Sagna, akiondoka na kusajiliwa bure huko aendako kwa kuwa ni
mchezaji huru
No comments:
Post a Comment