Pages

Monday, May 5, 2014

WANAJESHI WAWILI WA DRC KWENDA JERA KWA KOSA LA UBAKAJI


Wanajeshi wa DRC

Wanajeshi wawili wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepatikana na hatia ya ubakaji kati wanajeshi 39 walioshitakiwa kwa makosa ya kivita mashariki mwa nchi hiyo.
Wengine waliobaki wamepunguziwa makosa kutoka makosa ya uhalifu wa kivita lakini wamehukumiwa kwa makosa mengine kama vile uporaji lakini wengi waliachiwa.

 Wanajeshi wa DRC pichani.

Wanajeshi hao wanatuhumiwa kusababisha machafuko yanayoendelea kwenye mji mdogo wa Minova ulio mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2012.
Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23 .
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu wanawake na wasichana 135.
Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la mashariki mwa Congo na yanaidiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili waasi na wale wa serikali.

No comments:

Post a Comment