Zaidi ya washiriki 56 wanashiriki katika Kongamano la kujadili sekta ya uziduaji na uchanjuaji wa sekta ya madini mafuta na gesi katika sekta za sheria,kanuni,sera na mikataba kwa watendaji wa sekta hiyo kutoka kwenye nchi za jumuiya ya Afrika mashariki.
Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa kitengo cha madini kanda ya kaskazini(TMG) Mhandisi Gilay Shamika alisema kuwa kongamano hilo la siku mbili lilovuta wadau wa sekta ya madini kutoka nchi za Kenya Uganda na wenyeji Tanzania na kuandaliwa na taasisi ya Global Academy ya nchini Uingereza.
Shamika alisema kuwa sekta ya madini na gesi imekuwa na changamoto mbali mbali ambazo zinahitaji elimu na ufahamu wa hali ya juu kwenye Nyanja hiyo hivyo wanakutana kujadiliana kwa pamoja na wenzao kuweza kupata uelewa zaidi.
Aidha alisema kuwa wadau hao kutoka sekta za sheria,madini na fedha ndiyo wanahusika katika kongamano hilo huku wakipata uelewa ni jinsi gani watakavyoweza kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la taifa kutokana sekta ya madini hususani Mafuta na Gesi.
Giley alisema kuwa sekta ya madini hususani kwenye eneo la Mafuta na gesi limekuwa na changamoto mbali mbali hivyo ni sekta muhimu kuielewa kwa mapana hivyo wao na taasisi hiyo wanajadili kuweza kuzinufaisha nchi za ukanda huu.
No comments:
Post a Comment