Pages

Sunday, October 26, 2014

ALI KIBA AKANUSHA KUANDAA WATU KUMZOMEA DIAMOND PLATNUMZ

Alikiba amekanusha uvumi unaodai kuwa huenda aliaandaa watu maalum wa kumzomea Diamond Platnumz kwenye show ya Fiesta iliyofanyika October 18 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Alikiba amesema kuwa hajui uvumi huo umeanza vipi.
“Hamna ukweli wowote, naanzaje?,” amehoji. “Siwezi kufanya kitu kama hicho. Kikubwa ni kuwashukuru wana Dar es Salaam walivyonipokea, nimefurahi sana. Hii imenitia moyo na kunifanya niongeze bidii kuwaandalia vitu vizuri zaidi.”
Katika hatua nyingine, msanii huyo amesema mashabiki wa muziki wake wasishangae kuona video ya wimbo wa ‘Mwana’ wiki hii ama wiki ijayo. “Video ni muda wowote yaani, usishangae ukasikia video imetoka. Muda wowote video inatoka surprise, kwahiyo waendelee kusubiri muda wowote.”

No comments:

Post a Comment