Christopher Maurice "Chris" Brown.
MWIMBAJI mashuhuri duniani, Christopher Maurice "Chris" Brown ameonekana kuwakera mashabiki wake baada ya jana kutuma ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter kuhusu Homa ya Ebola na kutoa maoni yake.
Maoni aliyoandika Chris Brown.
Brown alindika hivi: ''Sijui, lakini nadhani janga la Ebola ni njia mojawapo ya kupunguza idadi ya watu duniani, janga hili linatisha kweli,''.
Ujumbe huo ulionekana kuwakera sana mashabiki wake ambapo baadhi walimjibu kuwa kama hana cha kusema bora akakaa kimya.
Muda mfupi baada ya staa huyo kubaini kuwa ujumbe wake huo umewakera watu aliandika hivi: ''Afadhali niwe kimya".
Homa ya Ebola mpaka sasa imesababisha vifo vya zaidi ya watu 4,000 katika ukanda wa Afrika Magharibi.
No comments:
Post a Comment