Pages

Tuesday, October 14, 2014

LORI LA MAFUTA LATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO MBAGALA RANGI TATU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA

Sehemu ya Mabaki Lori la mafuta lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo mara baada ya kupiga mweleka likiwa katika hatakati ya kulikwepa gari lingine lililokuwa likitokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani bila ya tahadhari,hali iliyolipelekea Lori hilo kukosa mwelekeo na kupiga mweleka.
Lori hilo pamoja na kupiga kwake mweleka halikuwa na madhara yeyote wala dalili ya kusema litawaka moto.Baada ya muda likaja kundi la vijana likiwa na madumu na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafura yaliyokuwemo kwenye lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa ulioliteketeza lori hilo.
haijafahamika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliepoteza maisha katika moto huo,ila hasara kubwa imeonekana kutokea kwa nyumba tatu zilikuwepo jirani na eneo la tukio zimeteketea kwa moto,ambazo moja ni ya makazi ya watu,duka la juma la Mchele pamoja nyumba ya kulala wageni.
Sehemu ya Lori hilo likiwa limeteketea kabisa.
Sehemu ya Wakazi wa Maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.
Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.
PICHA KWA HISANI YA MTAA KWA MTAA BLOG

No comments:

Post a Comment