Pages

Sunday, October 12, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE ALIFUNGUA RASMI DARAJA LA MALIGISU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete watatu kutoka kulia akiwa amekata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Maligisu. Wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akifatiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli

Taswira ya Daraja la Maligisu kama linavyoonekana kwa chini.
Daraja la Maligisu kama linavyoonekana kwa juu mara baada ya kufunguliwa
Pilikapilika mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Maligisu ambapo maelfu ya wakazi wa Kwimba na Magu walijitokeza katika sherehe hizo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakipita juu ya daraja hilo la Maligisu mara baada ya ufunguzi
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli. Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi

No comments:

Post a Comment