Bado haijulikani kama mchezaji matata wa Real Madrid Gareth bale atacheza katika mechi dhidi ya Liverpool katika ligi ya mabingwa ulaya hapo Jumatano.
Bale mwenye umri wa miaka 25 anauguza jeraha la misuli ya paja. Jeraha hili lilimpelekea kutoshiriki mechi ya Real madrid dhidi ya Levante Jumamosi licha ya kuratibiwa kama mchezaji wa ziada.
Taarifa iliyotelewa na Real Madrid haikufafanua muda ambao Bale atasali nje ya uwanja hata hivyo walisema atazidi kukaguliwa jinsi anavyopata nafuu.
Baada ya mechi yao ya Kundi B itakayochezewa ugani Anfield, Real Madrid inatarajiwa kukabana koo na mahasimu wao wa jadi Barcelona katika ligi ya El Clasico hapo jumamosi.
Bale aliichezea timu yake ya taifa ya Wale kwa vipindi vyote viwili dhidi ya Bosnia Hercegovina hapo tarehe 10 oktoba na kisha akaichezea tena dhidi ya Cyprus siku tatu zilizofuata katika michuano ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa ulaya.
Bale ambaye alihamia Real Madrid kutoka Tottenham mwaka uliopita kwa kima cha takriban pauni milioni 85.3, ameichezea real Madrid mechi 12 huku akiwa amefunga mabao matano
Chanzo:BBC Swahili
Chanzo:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment