Pages

Thursday, November 6, 2014

CHELSEA YATOKA SARE 1-1 UGENINI

CHELSEA imelazimishwa sare ya 1-1 ugenini na Maribor katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
Agim Ibraimi alitangulia kuifungia Maribor dakika ya 50, kabla ya Nemanja Matic kuisawazishia Chelsea dakika ya 73. 
Mshambuliaji Eden Hazard aliinyima Chelsea ushindi baada ya mkwaju wake wa penalti kuokolewa huko Slovenia. Matokeo hayo yanaifanya The Blues ifikishe pointi nane baada ya mechi nne, ikiendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Schalke 04 yenye pointi tano baada ya kufungwa 4-2 Sporting yenye pointi nne sasa. Maribor inashika mkia kwa pointi zake tatu. 
Kikosi cha Maribor kilikuwa: Handanovic, Stojanovic, Rajcevic, Arghus, Viler, Ibraimi/Bohar 90, Mertelj, Filipovic, Sallalich/Ndiaye dk90, Zahovic/Mendy dk73 na Tavares. 
Chelsea; Cech, Ivanovic, Zouma, Terry, Luis/Ramires dk56, Fabregas, Matic, Schurrle/Oscar dk46, Willian/Costa dk46, Hazard na Drogba.

No comments:

Post a Comment