Pages

Wednesday, November 19, 2014

JENGO MOJA KATIKA MJI MKONGWE ZANZIBAR LAANGUKA ASUBUHI LEO

Moja ya Jengo katika Mji Mkongwe linalomilikiwa na Ndg. Rashid Abass Imram, limeaguka leo asubuhi kutokana uchakavu wake na baadhi ya wananchi wanaokaa jirani na jengo hilo wamesema jengo hilo lilikuwa na ufa kwa muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati na mwenye nyumba hiyo, kutokana mvua zinazonyesha hivi sasa katika visiwa vya zanzibar zimesababisha jengo hilo kupata maji nakuta zake na kuanguka.

Mashuhuda wa ajali hiyo wasema jengo hilo limepata ajali hiyo wakati wa saa moja asubuhi leo ikitokea ajali hiyo kulikuwa hakuna watu wakiwa wamekaa baraza eneo hilo hutumika kwa wakaazi wa sokomuhoga kukaa jirani na maskani ya jozcorner, Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa ila kunasemekana kuna mtoto hakuonekana mpaka sasa wanashaka kuwa labda amefunika na kivushi hicho Harakati za Kikosi cha Uokozi cha Zimamoto Zanzibar wakiendelea na kuvukua kivusi hicho kuona kama kuna mtu amefukiwa na kifusi cha nyumba hiyo









Credits: ZanziNews

No comments:

Post a Comment