U
Heard ya jana alisikika Linex ambaye alilalamika kudhulumiwa pesa kiasi
cha milioni 11 na Nyamihela, ambaye alikutanishwa na muigizaji Steve
Nyerere ambapo Linex alisema lengo lake ilikuwa ni kununua gari na Steve
alimkutanisha na huyo jamaa kwa ajili ya kufanya biashara hiyo.
Leo amesikika Steve Nyerere ambapo
amesema yeye aliwakutanisha Linex na Nyamihela baada ya Linex kumwambia
kwamba anahitaji kununua gari, lakini baada ya hapo hakuwa na
mawasiliano tena na Linex.
Steve amesema Linex alimtafuta baada ya
kushindwana na Nyamihela na kumlalamikia Steve kwamba Nyamihela
kamdhulumu pesa ambayo alimpatia ili amuuzie gari, japo Steve amesema
kiasi cha pesa alichopatiwa Nyamihela ni milioni tatu na alimrudishia
milioni moja kati ya pesa hizo.
No comments:
Post a Comment