Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga walipata mabao yao yote kupitia kwa Simon Msuva katika dakika ya 73 na 90.
Kabla ya mechi hiyo, Yanga ilikuwa imepoteza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Licha ya kumkosa nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro', Yanga ilionyesha soka safi huku soka lake likiwa ni la kuvutia.
Mgambo nao walikuwa wakipeleka mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga lakini hawakuwa makini kwenye umaliziaji.
No comments:
Post a Comment