Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni
mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati
alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Novemba
15, 2014 kwa ajili ya kuzungumzia juu ya suala zima la maelekezo ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu uchaguzi Serikali za mitaa 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni
mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
na baadhi ya Wajumbe wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati akiondoka
kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Novemba 15, 2014
baada ya kuzungumza na wajumbe wa CCM juu ya suala zima la maelekezo ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu uchaguzi Serikali za mitaa 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni
mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta
jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida,
wakati wa mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam kuzungumzia suala zima la maelekezo ya Halmashauri Kuu ya
Taifa kuhusu uchaguzi Serikali za mitaa 2014.
Baadhi ya wajumbe wa CCm Mkoa wa Dar es Salaam, wakishangilia wakati
Mlezi wa CCM mkoa wao Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akizungumza
nao leo.
No comments:
Post a Comment