Pages

Saturday, November 1, 2014

MANENO ALIYOSEMA CHIDI BENZ KUHUSU RAY C BAADA YA KUACHIWA KWA DHAMANA

Rapper Chidi Benz ambae alishikiliwa na Polisi mwezi huu baada ya kukutwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akisafiri kwenda Mbeya, ameachiwa kwa dhamana na sasa yuko mtaani.
Mtangazaji wa So so Fresh ya Clouds FM Dj Fetty Ijumaa ya October 31 2014 alirushaExclusive interview na Chidi Benz ambae moja ya vitu alivyozungumza ni ishu ya kumpiga mwimbaji Rehema Chalamila a.k.a Ray C.

Soudy Brown ambae ni producer wa show hiyo alianza kwa kumuuliza Chidi…… ‘Ray C anasema ametupa kesi aliyokuwa amekufungulia’ Chidi akajibu >>> ‘Thanks kama ametupa hiyo kesi lakini sidhani kama kesi ilikua bado ipo kwa sababu mara ya mwisho nilimwambia points kadhaa ambazo zilikua ni za msingi, nilimtumia msg kwenye simu yake…. pls tuachane na huu ujinga, sanasana watu watakua wanatuona wale Wateja labda wamezinguana‘
‘Unasema nini Ray C wakati mimi ni mtu nimekuandikia miziki, nimerekodi na wewe…. mtu ulikua unaniambia unanipenda unasema Chidi jamani naomba nishoot video na wewe najua siwezi kukulipa, wewe kaka yangu kabila moja…. mtu nimekusaidia tumefanya vitu vingi, inawezekana vipi nije kukubadilikia na kuwa adui yako? ni kitu wewe umefanya unachokijua wewe lakini dunia haijui, watu hawajui mambo yetu…. hiyo ni mambo binafsi’

‘Hizo ni ishu zetu, kama unasema mimi ni kaka yako si mimi umeniudhi kaka yako kinyumbani….. so wewe umekuja kuchukua ukaleta kwenye media ukasema nimekupiga lakini mimi najua ulichokifanya na nilikukanya kwa mara ya kwanza ukaomba msamaha alafu mara ya pili ukafanya tena, nikakufata kwako kweli…… ‘
‘Mi najua Ray C yuko kwenye kuacha madawa anakunywa zile Methodone, najua madawa sio kitu kizuri…. mimi pia nilitumia kwa hiyo huwezi kuwa sawa kwa harakaharaka, unakua unapona taratibutaratibu, so najua alipitiwa tu….. point nyingine nilimwambia sidhani kama mimi ndio mtu mbaya sana kwako Ray C’
‘Nilimwambia kama ni kunikamata na kunipeleka jela nahisi kuna watu Ray C inatakiwa uwakamate na uwafunge jela hao ndio wamekuharibia sehemu kubwa ya maisha yako, hakuna kibaya nilichokufanyia mimi’ – Chidi Benz.


No comments:

Post a Comment