Mwanariadha wa mbio za marathon kutoka Kenya Rita Jeptoo amepatikana kuwa alitumia dawa za kusisimua misuli zilizopigwa marufuku.
Jetoo alifanyiwa uchunguzi nchini Kenya mnamo mwezi Septemba wiki mbili kabla ya kushinda mbio za Chicago marathon kwa mwaka wa pili mfululizo.
Chama cha riadha nchi Kenya AK kimelezea kughadhabishwa na matokeo hayo.
Jeptoo aliye na umri wa miaka 33 alitarajiwa kukabidhiwa kitita cha dola nusu milioni mjini New York siku ya Jumapili kutokana na ushindi huo lakini sasa sherehe hizo zimehairishwa.
Credits: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment