Maafisa
saba wa juu wa shirikisho la soka duniani, FIFA wamekamatwa kwa shutuma
za kupokea rushwa. Maafisa hao walikamatwa kwenye hoteli ya Baur au Lac
ya jijini Zurich, Jumatano hii. Polisi wa Uswisi wamekamata maafisa hao
wakiwemo makamu wa rais wawili baada ya kuivamia kwa kushtukiza hoteli
hiyo.
Makamu
wa rais wa FIFA, Jeffrey Webb anaaminika kuwa mmoja wa maafisa
waliokamatwa alfajiri ya leo wakiwa kwenye hoteli ya kifahari nchini
Uswisi
Eduardo Li, kutoka Costa Rica naye pia alikamatwa kwenye hoteli hiyo ya kifahari
Hatua
hiyo imekuja kufuatia upelelezi uliofanywa na Marekani kwa kipindi cha
miaka mitatu. Waendesha mashtaka wa Marekani wametoa hati za kukamatwa
kwa maofisa 14, kwa madai yakiwemo kutakatisha fedha haramu, ulaghai na
mengine.
Madai hayo ni pamoja na maafisa wa FIFA kupokea rushwa ifikayo dola milioni 150.
Mamlaka
za Uswisi zimefungua upelelezi tofauti wa jinai katika utendaji wa FIFA
kuhusiana na nafasi za kuandaa makombe ya dunia ya mwaka 2018 na 2022
zilizoenda kwa Urusi na Qatar.
Rais wa FIFA Sepp Blatter si miongoni mwa wanaoshtakiwa lakini alikuwa mmoja wa maafisa waliokuwa wakichunguzwa.
Uchaguzi wa FIFA utaendelea kama ulivyopangwa Ijumaa hii na pia michuano ya kombe la dunia nchini Urusi na Qatar haitaathirika.
No comments:
Post a Comment