Pages

Tuesday, November 4, 2014

RATIBA YA VIKAO VYA BUNGE MJINI DODOMA


Kufuatia uwepo wa Bunge Maalum la Katiba lililomalizika mwezi Oktoba, Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kumi na Sita na wa Kumi na Saba ilipangwa kufanyika kwa pamoja kuanzia tarehe 4 – 28 Novemba, 2014 mjini Dodoma.
Kazi zitakazofanyika katika mikutano hiyo ni pamoja na Bunge kukaa kama Kamati ya Mipango kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 94(1) na kupokea, kujadili na kutoa maoni na ushauri kuhusu bajeti ya serikali, vyanzo vya mapato pamoja na mapendekezo ya utekelezaji wake.Aidha kutakuwa na kusomwa kwa mara ya pili na hatua zake zote kwa miswada ya Sheria ya Serikali ambayo ilikwishasomwa kwa mara ya kwanza katika mikutano iliyotangulia; Muswada Binafsi wa Mbunge na Muswada Binafsi wa Kamati kama ifuatavyo:
A.Miswada ya Sheria ya Serikali
i.Muswada ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani wa Mwaka 2014. [The Value Added Tax Bill, 2014]

ii.Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2013. [The Statistics Bill, 2013].
iii.Administration Bill, 2014]

iv.Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2014 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2014] na,
v.Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014. [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2014]
B.Muswada Binafsi wa Mbunge
Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana wa Mwaka 2013. [The Youth Council Bill, 2013]
C.Muswada Binafsi wa Kamati
Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014. [The Budget Bill, 2014].
Aidha, Bunge litapokea taarifa ya Kamati Teule iliyoundwa tarehe 1/11/2013 ili kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo, maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi.
Pamoja na mambo mengine, Bunge pia litajadili maazimio matatu ambayo ni:
i. Azimio la kuridhia Itifaki ya Afrika Mashariki Kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Kiulizi. [The East African Protocol on Cooperation in Defence Affairs].

ii. Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia makubaliano ya msingi ya Ushirikiano katika Bonde la Mto Nile, [Agreement on the Nile River Basin Co-operative Framework – CFA]
iii. Azimio la kuridhia Itifaki ya Uzuiaji wa Vitendo Haramu dhidi ya Usalama wa Miundombinu ya kudumu iliyojengwa chini ya Bahari katika mwambao wa Bara ya mwaka 1988.[The Protocol for the Suppression of Unlawful Acts against the Safety of Fixed Platforms located on the Continental Shelf – SUA, 1988].

Aidha, kutakuwa na maswali ya kawaida kwa mujibu wa kanuni ya 39(1) ambapo kwa mikutano hii miwili yakuwa 265 na maswali kwa Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni ya 38(1).
Mwisho Waheshimiwa Wabunge wakiwa Dodoma watapata fursa ya kushiriki semina mbalimbali za kujenga uwezo katika nyanja za kilimo na usalama wa chakula; faida za ushirikiano katika Bonde la Mto Nile; na umuhimu wa kupima/kuchunguza afya mara kwa mara.
Ratiba ya Mkutano itatolewa mara baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi kitakachofanyika tarehe 4 Novemba 2014, Dodoma.

No comments:

Post a Comment