Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC, wakivuka barabara kurejea tena
ofisini baada ya kuzikimbia kutokana na hitilafu ya umeme iliyotokea
kwenye lifti ya dharula katika Makao Makuu ya benki hiyo, makutano ya
mitaa ya Sokoine Drive na Azikiwe, Dar es Salaam leo. Hitilafu hiyo
iliyotokea majira ya saa 3:30, ilisababisha tafrani kiasi cha
wafanyakazi kuzikimbia ofisi kwenda Bustani ya Posta ya Zamani (picha
ndogo).Wateja waliopatwa na zahama hiyo walielekezwa na uongozi kwenda
kupata huduma kwenye matawi mengine ya benki hiyo. (PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Wafanyakazi wakiwa kwenye bustani ya Posta ya Zamani iliyopo mbele ya jengo lao, baada ya kumbia tafrani hiyo
Wafanyakazi wa Benki hiyo wakirejea ofisini baada ya kuhakikishiwa usalama majira ya saa 4;35 asubuhi
Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wakiwa na vifaa vyao tayari kutoa
huduma hiyo. Hata hivyo kwa mujibu wa Rukia Mtingwa alisema hakuna
mfanyakazi wala mteja aliyeumia wakati wa tafrani hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa
(katikati) akiwasilinana na watu mbalimbali baada ya hali ya usalama
kurejea
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (wa pili
kulia) akizungmza na waandishi wa habari juu ya tafrani hiyo.
No comments:
Post a Comment