Moja ya story ambazo zilichukua uzito wa juu katika vyombo vya habari wiki iliyopita ilikuwa ni kitendo cha yule mama mfanyakazi wa Chama cha Republican Marekani, Elizabeth Lauten ambaye alikuwa kitengo cha Mawasiliano kukosoa mavazi ya watoto wa Obama bado ni story inayoendelea kuzungumziwa.Mama huyo aliwaponda Sasha na Malia kuwa wamekosa ustaarabu kutokana na kuvalia sketi fupi katika hafla ya chakula katika Ikulu ya White House, pia alisema kuwa watoto hao ni kama hawakuwa na nyuso za furaha kuwa katika hafla hiyo, ambapo baada ya kushambuliwa na watu kwenye ukurasa wake wa Facebook aliomba radhi, na baadaye akajiuzulu.
Leo ni siku ya nne tangu amejiuzulu lakini story ni kwamba bado ameendelea kufuatiliwa na vyombo habari, huku wengine wakipiga kambi nyumbani kwa wazazi wake kuchunguza vitu mbalimbali ikiwemo rekodi ya maisha yake ya utotoni ambapo watu kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa kwa kusema hiyo haikuwa ‘big deal’ ya kufanya vyombo vya habari kumfuatilia kiasi hicho.
No comments:
Post a Comment