Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan
amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia
ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa
amelewa mjini Mumbai.
Khan
alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari
lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya
barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa
katika ajali hiyo.
Khan
amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda
wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada
ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Jaji wa mahakama hiyo, Khan anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Credit: BBC
No comments:
Post a Comment