Mke wa Rais wa Nigeria, Mrs Buhari akiwa na mabinti zake
KILENDEMO's BLOG
Monday, June 1, 2015
PICHA YA MKE WA RAIS MPYA WA NIGERIA AKIWA NA MABINTI ZAKE
Friday, May 29, 2015
SEPP BLATTER ASHINDA TENA URAIS WA FIFA
Sepp Blatter baada ya ushindi.
Blatter akiwa na mpinzani wake Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan.
SEPP Blatter ameshinda tena Urais wa FIFA kwa awamu ya tano baada ya
kumshinda mpinzani wake Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan.
Blatter amepata kura 133 dhidi ya 73 za mpinzani wake huyo katika
raundi ya kwanza ya kinyang'anyiro hicho kilichofanyika nchini Uswizi
leo licha ya kukumbwa na skendo za ufisadi.
MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA AAPISHWA NA MKUU WA MKOA WA DODOMA LEO
Mhe.
Athony Mavunde akila kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mbele ya
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Hayupo Pichani) Mei 29,2015
Mhe.
Athony Mavunde akitia saini hati ya kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa Mei 29, 2015
Mkuu wa
Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto) akipongezwa na baba yake
mzazi Ndg. Peter Mavunde mara baada ya kula kiapo cha kuwa Mkuu wa
Wilaya Mei 29,2015
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto kwake)
na wajumbe wa kamatiya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma wakati wa Hafla
ya kumuapisha Mkuu huyo mpya wa Wiaya ya Mpwapwa Mei 29,2015
Thursday, May 28, 2015
MAAFISA WA FIFA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Maafisa
saba wa juu wa shirikisho la soka duniani, FIFA wamekamatwa kwa shutuma
za kupokea rushwa. Maafisa hao walikamatwa kwenye hoteli ya Baur au Lac
ya jijini Zurich, Jumatano hii. Polisi wa Uswisi wamekamata maafisa hao
wakiwemo makamu wa rais wawili baada ya kuivamia kwa kushtukiza hoteli
hiyo.
Makamu
wa rais wa FIFA, Jeffrey Webb anaaminika kuwa mmoja wa maafisa
waliokamatwa alfajiri ya leo wakiwa kwenye hoteli ya kifahari nchini
Uswisi
Eduardo Li, kutoka Costa Rica naye pia alikamatwa kwenye hoteli hiyo ya kifahari
Hatua
hiyo imekuja kufuatia upelelezi uliofanywa na Marekani kwa kipindi cha
miaka mitatu. Waendesha mashtaka wa Marekani wametoa hati za kukamatwa
kwa maofisa 14, kwa madai yakiwemo kutakatisha fedha haramu, ulaghai na
mengine.
Madai hayo ni pamoja na maafisa wa FIFA kupokea rushwa ifikayo dola milioni 150.
Mamlaka
za Uswisi zimefungua upelelezi tofauti wa jinai katika utendaji wa FIFA
kuhusiana na nafasi za kuandaa makombe ya dunia ya mwaka 2018 na 2022
zilizoenda kwa Urusi na Qatar.
Rais wa FIFA Sepp Blatter si miongoni mwa wanaoshtakiwa lakini alikuwa mmoja wa maafisa waliokuwa wakichunguzwa.
Uchaguzi wa FIFA utaendelea kama ulivyopangwa Ijumaa hii na pia michuano ya kombe la dunia nchini Urusi na Qatar haitaathirika.
Thursday, May 14, 2015
PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAZISHI YA MTOTO WA BABA WA TAIFA
Askofu
wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila akisali
mbele ya jeneza la marehemu John Guido Nyerere kabla halijaingia
kanisani kwa ajili ya ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki
la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya
Butiama.
Viongozi
na wananchi wakishiriki ibada ya kumuombea marehemu John Gaudo Nyerere
katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la
Musoma Parokia ya Butiama
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila
akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Guido Nyerere baada ya kukamilika kwa ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki
la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya
Butiama.
akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Guido Nyerere baada ya kukamilika kwa ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki
la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya
Butiama.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa
Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa wakati wa
mazishi ya John Guido Nyerere yaliyofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa
,Butiama.
Jeneza
lenye mwili wa marehemu John Guido Nyerere likiteremshwa kaburini na
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mama Maria Nyerere akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akiweka udongo kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
Mtoto
wa mwisho wa marehemu John Guido Nyerere anayefahamika kwa jina la
Wanzagi akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na shangazi yake Anna
Nyerere.
Ni huzuni kwa kila mtu.
Mama Maria Nyerere akiweka shada la mau kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
Mtoto
wa Marehemu anayeishi Lusaka Zambia, Sofia Nyerere Mwape akiweka shada
la maua kwenye kaburi la Baba yake marehemu John Nyerere.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima mbele ya kaburi la
marehemu John Gaudo Nyerere mara baada ya kuweka taji la maua.
Mbunge
wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akiweka shada la
maua kwenye kaburi la marehemu John Nyerere kwenye mazishi yaliofanyika
nyumbani kwa marehemu Baba wa Taifa Butiama.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishiriki kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
Baadhi ya Watoto wa marehemu pamoja na ndugu wengine.
Mheshimiwa
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akisoma salaam za rambi
rambi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wakati wa mazishi ya
John Nyerere.
Emily Magige Nyerere akifafanua jambo wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere.
Wednesday, May 6, 2015
SALMAN KHAN AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO KWA MAUAJI
Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan
amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia
ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa
amelewa mjini Mumbai.
Khan
alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari
lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya
barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa
katika ajali hiyo.
Khan
amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda
wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada
ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Jaji wa mahakama hiyo, Khan anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Credit: BBC
Subscribe to:
Posts (Atom)