Pages

Wednesday, April 2, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE ! CHELSEA NA PSG VITANI , WAKATI REAL MADRID NA BORUSSIA DORTMUND HAPATOSHI.

 
Mourinho: Chelsea are out of the title race
                                                             Jose Mourinho

LEO ndiyo leo, mchuano wa hatua ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya inaendelea tena leo katika viwanja viwili tofauti ambapo Borussia Dortimund ya Ujerumani inavaana na Real Madrid ya nchini Hispania kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park uliopo nchini Hispania.
Mbali na mtanange huo, timu ya Paris St. German (PSG) itakutana na Chelsea ya Uingereza katika kipute kinachofanyika kwenye Uwanja wa Parc des Princess nchini Ufaransa ambapo Chelsea wamesafiri kwenda nchini humo kwa ajili ya mtanange huo.
Tayari 'wazee wa kubeti' kamari wameweka mamilioni ya shilingi katika kubahatisha bingwa baina ya timu hizo mbili kubwa pambano linalotolewa macho ni la Chelsea kutokana na ligi hiyo kuwa na mashabiki wengi nchini na kwingineko duniani.
Timu hizo ambazo zote zinawategemea mastaa wao katika kuhakikisha wanafanya vyema, zitakuwa na upinzani mkali huku kila kikosi kitaka kuweka historia kutokana na kuheshimika kwa ligi hiyo kubwa barani Ulaya.
Mechi ya kati ya Chelsea na PSG inatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu zote kucheza mchezo wa kasi na wa mashambulizi, jambo linalotoa utabiri mgumu wa nani anaweza kuibuka mbabe katika kipute hicho.
Licha ya wadadisi wa soka, kueleza kuwa kuna tofauti kubwa ya aina ya uchezaji kwa timu za Uingereza na Ufaransa bado ubashiri kwa timu zote umekuwa na hasi kutokana na kucheza kwa viwango tofauti kimchezo.
Kwa mujibu wa Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alikiri kuwepo katika wakati mgumu kutokana na mahesabu yake kuelekeza katika kinyang'anyiro cha Ubingwa wa Ligi Kuu, Uingereza kwa ajili ya kuweka heshima zaidi.
Kwa upande wake, mchezaji tegemezi wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anatagemewa kufanya maajabu katika mechi ya leo dhidi ya Borrusia kutokana na kasi yake uwanjani, licha ya klabu yake kuwa katika kiwango kizuri msimu huu.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana jumla ya mabao 28 katika ligi ya La Liga, pia ametupia jumla ya mabao 13 katika fainali hizi za kombe la Klabu Bingwa Ulaya.
Mchezaji Robert Lewandowski wa Dortimund anatarajiwa kuwa mwiba wa kuotea mbali, baada ya kufanikiwa kuisambaratisha Madrid katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita, licha ya kuwapo kwa taarifa za majeruhi ya goti wiki hii.
Hata hivyo Meneja wa Dortimund, Jurgen Klopp amesema huenda nafasi hiyo ikajazwa na Marco Reus, huku akitamba kuzifanyia maajabu timu za Hispania kutokana na kuwa na kikosi chenye ari na ushindi wa hali na mali.
PSG inamtegemea mno kiungo wake mshambuliaji, Zlatan Ibrahimovic kama Mungu wao kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao ndani ya ligi hiyo na hata kwenye timu ya taifa ya Sweden.
Mshambuliaji huyo mwenye uwezo na kasi ya hali ya juu, huenda akatoa upinzani mkali kwa mashabiki timu pinzani kutokana na aina yake ya uchezaji, pindi awapo uwanjani hivyo huwasumbua mabeki kwa kiwango kikubwa.
Ibrahimovic anategemea kushirikiana kikamilifu na mchezaji mwenzake, Edinson Cavani raia wa Uruguay ambaye ataongeza safu ya mashambulizi kwa timu pinzani huku kila mmoja akikubalika kutokana na uwezo wake katika nafasi yake.
Mechi zote hizo zinachezwa saa 3.45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika muda unaofanana hivyo wazee wa kubeti wana wakati mgumu kubashiri matokeo ya leo ambapo marudio yatafanyika wiki mbili zijazo.

Source: Majira

No comments:

Post a Comment