Demba Ba akiifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 45 ya mchezo.
Ba na Sakho wakichuana.
TIMU ya Liverpool imepokea kipondo cha bao 2-0 kutoka kwa Chelsea
katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Uwanja wa Anfield jijini
Liverpool leo.
Mabao ya Chelsea yamewekwa kimiani na Demba Ba dakika ya 45 wakati la pili likifungwa na Willian dakika ya 90.
Kwa matokeo ya leo, Chelsea wamefikisha pointi 78 wakiwa nafasi ya
pili baada ya kucheza mechi 36 wakati Liverpool wakibaki kileleni na
pointi 80 wote wakisalia na mechi mbili kumaliza ligi.
No comments:
Post a Comment