Jana tarehe 7, ni miaka miwili tangu afariki Steven Kanumba, muigizaji aliyeacha
pengo kubwa kwenye tasnia ya filamu Tanzania na Afrika mashariki kwa
ujumla.
Aliyekuwa muigizaji mwenzake aliyeshirikiana nae katika kazi ya
uigizaji wa filamu tangu akiwa mdogo, Elizabeth ‘Lulu’ Michael amepost
video yenye picha kadhaa za Kanumba na za kwake na ameandika ujumbe
maalum kwa ajili yake.
“Bado siamini Kama mwaka wa pili unakatika bila kukuona wala
kukusikia baba…!Ninaamini bdo tupo wote kiroho na Ninaamini zaidi nafsi
yako huko ilipo inasimama kunitetea na kunipigania,inaweza kunichukua
miaka na miaka kukuelezea….u still liv in me daddy and your dearly
missed….R.I.P daddy angu.” Ameandika Lulu
No comments:
Post a Comment