Rwanda imeanza rasmi wiki moja ya maombolezo
kukumbuka miaka 20 tangu kutokea kwa mauji ya kimbari. Rais Paul Kagame
aliwasha mwenge ambao utawaka kwa siku 100 – muda sawa na mauaji
yalivyodumu.
Mzozo wa kidiplomasia umezuka baina ya Rwanda na Ufaransa na hata umesababisha balozi wa Ufaransa nchini humo, Michel Flesch, asihudhurie shughuli hizo.
Wengi wa walioathirika walikatwa kwa mapanga katika mauaji yaliyoanza 6 Aprili 1994, muda mfupi baada ya Rais Juvenal Habyarimana ambaye alikuwa mhutu kuuawa wakati ndege ilipotunguliwa katika anga ya mji mkuu Kigali.
uko vizuri brother
ReplyDelete