Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akizungumza na shangazi wa mtoto
aliyeibiwa pembeni ni baadhi ya waandishi wa habari walioshuhudia
makabidhiano hayo.
BAADA
ya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kumtia nguvuni Askari wake
anayetuhumiwa kuiba mtoto wilayani Kyela,Mtoto huyo akabidhiwa kwa
wazazi wake huku wakiendelea na uchunguzi zaidi.
Makabidhiano
hayo yamefanyika katika Hospitali ya Wazazi Meta alikokuwa akipatiwa
matibabu mtoto huyo katika chumba cha Joto na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Ahmed Msangi.
Akipokea
Mtoto wake Mama mzazi Mboka Mwakikagile(20) amelishukuru Jeshi la
polisi na wananchi wema kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto wake
Goodluck Salehe aliyeibwa na Askari wa Jeshi la Polisi WP 5367 Prisca
Kilwai April 6, mwaka huu huko Kasumulu wilayani Kyela.
Aidha
mwanamke huyo amemshukuru zaidi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed
Msangi pamoja na Askari wengine waliofanikisha mtoto wake kupatikana
akiwa hai.
Baadhi
ya ndugu waliofurika katika Hospitali ya Meta kushuhudia makabidhiano
hayo wamesema hawaamini kile kilichotokea baada ya kuwa katika hofu
takribani siku kumi na moja baada ya kuibwa katika zahanati ya Njisi
iliyopo Kasumulu Kyela.
Aidha
ndugu hao wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kupatikana
mtoto na wasamaria wote walioshirikiana nao katika maombi hata
kufanikisha upatikanaji wa mtoto huyo akiwa salama salimini.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,akizungumza
baada ya kukabidhi mtoto huyo aliwasihi wazazi kuwa makini na utunzaji
wa watoto ili kuepuka vitendo kama hivyo kujirudia.
Ameongeza
kuwa Jeshi la polisi bado linafanya upelelezi na kukusanya ushahidi
zaidi ili waweze kuwafikisha mahakamani watumiwa kujibu mashtaka
wanayokabiliana nayo.
Amesema
Mtoto huyo alipatikana Aprili 17, mwaka huu akiwa na Askari huyo majira
ya saa nne asubuhi na kuongeza kuwa mpaka sasa sababu za kuiba mtoto
huyo hazijafahamika na atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya
kuhukumiwa kijeshi.
|
No comments:
Post a Comment