Pages

Sunday, April 27, 2014

NGORONGORO HEROES YAIFUNGA TIMU YA VIJANA YA KENYA KWA PENALTI 4-3



Mshambuliaji wa Ngorongoro, Ally Bilal (kulia) akichuana na beki wa Kenya, Geofrey Shivekwa, wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za michuano ya Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, zinazotegemea kufanyika mwakani nchini Senegal. 


Iddi Suleiman  wa Ngorongoro (kulia) akichanja mbuga.


Wachezaji wa Ngorongoro, wakishangilia ushindi baada ya kushinda kwa penati na kusonga mbele

TIMU ya soka ya taifa ya Vijana U20, Ngorongoro Heroes jioni hii imewafuta machozi Watanzania baada ya kuiodnosha patupu timu ya Kenya kwa kuifunga mkwaju ya penati 4-3 katika mechi ya kuwania kucheza Fainali za Afrika.
Ngorongoro imepata ushindi huo baada ya kushindwa kutambiana na vijana wenzo katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni siku moja tangu kaka zao kunyukwa 3-0 na Burundi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kuadhimisha sherehe za Muungano.
Katika mechi hiyo Tanzania ilipata penati kupitia kwa Kevin Friday, Mohammed Hussein, Mange Chagula na Iddi Suleiman, huku Mudathir Yahya alikosa yake.
Wakenya walipata penati zao kupitia Geofrey Shiveka, Timonah Wanyonyi na Victor Ndinya, huku Evans Makari na Harison Nzivo walipoteza.

Kwa kufuzu huko Tanzania sasa inatarajiwa kuvaana na Nigeria katika hatua inayofuata katika kuwania kucheza fainali hizo zitakazofanyika nchini Senegal. 

No comments:

Post a Comment