Pages

Saturday, April 26, 2014

PICHA MBALI MBALI KWENYE SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZILIZOFANYIKA UWANJA WA UHURU

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
 Viongozi mbalimbali wakifuatilia maadhimisho hayo. 
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru leo.
 Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.
 Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride...
 Paredi la askari....likiwa ni tofauti na ilivyozoeleka...
 Moshi wa rangi...
 Ndege za kijeshi zikipita kwa speed ya ajabu...
 Askari wa Jeshi akishuka kwa Parachuti....
 Askari wa Miamvuli wakishuka kutoka umbali wa Futi 4000.....
 Watoto wa Halaiki...
Wasanii wa miziki tofauti tofauti 50, walioshirikiana kuimba wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment