- Cheka atoka sare, Miyeyusho achapwa raundi ya kwanza.
Bondia Fransic Cheka (kushoto) akichapana na Gavad
Zohrehvand wa Iran wakati wa pambano lao la Kimataifa la kirafiki
lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam jana
usiku. Katika pambano hilo mabondia hao walitoka droo ya kufungana
point.
Bondia Fransic Cheka (kushoto) akiliana 'timing' na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa pambano lao.
Bondia Fransic Cheka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao.
Bondia Sukkasem Kietyongyuth
kutoka Thailand (kulia) akimkalisha bondia Fransic Miyeyusho, katika
raundi ya kwanza ya pambano lao la raundi kumi na kumaliza pambano hilo
kwa KO.
Bondia Fransic Miyeyusho (kushoto) akijitutumua kuendelea kupigana na Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutokaThailand. Katika pambano hilo Miyeyusho alipigwa raundi ya kwanza kwa K.O.
Bondia
Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kushoto) akimwadhibu Mustafa Dotto
wakati wa pambano lao la utangulizi lililofanyika katika ukumbi wa PTA
Sabasaba jana usiku jijini Dar es salaam. Katika pambano hilo King class
alishinda kwa pointi.
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kushoto) akiendelea kumwadhibu Mustafa Dotto. |
No comments:
Post a Comment