Ahadi hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Uingereza,
David Cameron wakati akizungumza ofisini kwake 10 Downing Street na Rais
Jakaya Kikwete, ambaye yupo nchini humo kwa ziara ya siku tatu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu, Waziri Mkuu
Cameron pia alijivunia nchi yake kwa kuongoza kwenye sekta ya uwekezaji
nchini humu.
“Tunakaribia mwisho wa muda wa Malengo ya Milenia
Mwaka 2015, tutahitaji kuweka vipaumbele vingine baada ya hivyo kama
kuondoa umaskini, majisafi na salama, masuala ya ufisadi na utawala
bora,” alikaririwa Cameron katika taarifa hiyo.
“Natumaini utaendelea kutoa mchango wako baada ya
malengo hayo kufikia tamati,” alisema Waziri Mkuu Cameron, pia Rais
Kikwete amekubali ombi hilo na kuahidi ushirikiano wake.
Akizungumzia kuhusu uwekezaji, Cameron ameahidi
kuendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta
maendeleo.
Rais pia alipata fursa ya kufungua mkutano kuhusu
uwekezaji, ambako aliitumia kuelezea nafasi za uwekezaji nchini Tanzania
na vivutio mbalimbali vilivyopo.
“Fursa ni nyingi, amani, usalama, soko la kutosha
na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda
wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc),
hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana,” alisema Rais Kikwete.
Rais pia amekutana na Watanzania waishio huko, na
kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa Jiji la London, Mama Alderman
Fiona Woolf, ambaye ameahidi kutembelea Tanzania, Septemba mwaka huu.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment