KATIKA hali isiyo ya
kawaida, wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba jana walijikuta wakipokewa
kwa mabango baada ya wananchi kuandamana katika kumbi mbalimbali
walizopangiwa kufanyia vikao vya kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba,
mjini Dodoma.
Maandamano hayo yalikuwa na ujumbe uliokuwa na lengo la kuwashinikiza wajumbe hao kutochakachua maoni yaliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji mstaafu Joseph Warioba, wakati wakijadili rasimu hiyo.
Moja ya mabango hayo lilisomeka; "Katiba Mpya.
Akinamama wenzetu mlioingia kwenye Bunge la Katiba msikubali maoni ya wananchi kuchakachuliwa".
Lingine likisomeka; "Bahati mbaya sana kuona nyongeza ya wajumbe 201, inashindwa kutetea maoni ya wananchi wanaowawakilisha".
Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wananchi hao walisema waliamua kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa wajumbe hao waweze kuijadili rasimu kwa makini.
Mmoja wa wananchi hao ambaye alijitambulisha kwa jina la Benadeta Mwaluko, alisema lengo lao ni kutaka wajumbe wa Bunge hilo wafahamu kuwa wananchi ndio waliowatuma kwenda kuwawakilisha si vyama vyao.
Alisema hawapo tayari kuona Rasimu iliyotolewa na tume ya Jaji Warioba inachakachuliwa kama ilivyopangwa na baadi ya wajumbe hivyo kuwataka waheshimu maoni ya wananchi badala ya kuyapinga kwani tume hiyo iliundwa na Rais Jakaya Kikwete na kufanya kazi ya kukusanya maoni nchi nzima.
"Kama maoni ya wananchi yatachakachuliwa, tutaikataa rasimu ambayo itapitishwa na wajumbe kwa kupiga kura," alisema.
Mwananchi mwingine, Kahumba Leula alisema wamepoteza imani na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Bw. Samuel Sitta tofauti na awali kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge hilo.
Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo wameona ni vyema wafikishe ujumbe kwa njia hiyo ili kuwakumbusha wajumbe kuwa wananchi wanawafuatilia hivyo wasichakachue rasimu hiyo.
Aliwataka baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kutomshambulia Jaji Warioba kwa kuwasirisha rasimu hiyo kwani kile alichokisema ni mawazo ya wananchi na si mawazo yake binafsi.
Kutokana na tukio hilo la aina yake, Jeshi la Polisi mkoani humo, linawashikilia watu watatu kwa kosa la kuhamasisha uvunjifu wa amani.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo, David Misime, alisema tukio hilo lilitokea saa 3:30 asubuhi ambapo watu hao walifanya mkusanyiko usio halali.
"Watu hawa walibeba mabango yaliyolenga kuhamasisha uvunjifu wa amani katika kumbi mbalimbali ambazo wajumbe wa Bunge la Katiba wanajadili Rasimu ya Pili ya Katiba," alisema.
Kamanda Misime aliwataja watu waliokamatwa kuwa ni Agustino Pancras (60), Cosmas Katebeleza (44) na Jotam Tarukundo (35), wote wakazi wa Manispaa ya Dodoma.
Alisema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi ukikamilika kulingana na ushahidi kwa kosa hilo na kuongeza kuwa, jeshi hilo linaendelea kuwatafuta wengine ili waweze kuwachukulia hatua za kisheria.

Chanzo: Majira
No comments:
Post a Comment