1. Agnes Masogange
Huyu
alijipatia bahati ya kufahamika kwa kasi baada ya msanii belle 9
kumtumia kwenye nyimbo yake ya masogange ambayo Agnes alicheza kama
Masogange, hadi Leo anafahamika kwa jina la masogange, ni kati ya watu
wanaozungumzwa sana mitandaoni. Kesi yake ya madawa ya kulevya ilimuweka
kwenye ulimwengu wa mastaa.
2. Romy Jones
Huyu
jamaa ni ndugu wa Diamond. Amefahamika sana baada ya kuwa karibu na
mwanamuziki Huyo, japokuwa ana maringo na nyodo kuzidi Diamond. Na yeye
huyu sio mwanamuziki wala mcheza filamu.
3.Penny
Huyu
bidada ni mtangazaji wa Dtv. Alikuwa hafahamiki apo awali, Jina lake
lilivuma sana na kujikuta akiingia kwenye ulimwengu wa mastaa baada ya
kujihusisha kimapenzi na msanii Diamond, ni miongoni mwa watu
wanaofuatiliwa sana na kuzungumzwa.
4.Mange kimambi
Huyu
alipata umaarufu kupitia mastaa kadhaa wa Tasnia mbali mbali apa bongo,
alianza kuzinguana kwenye blogs na msanii wa maigizo Sintah, Ray(
kuhusu kifo cha Kanumba), Shigongo na wengine kadhaa, wengi walitaka
kumjua ni mtu wa aina gani baada ya kuanzisha bifu na mastaa wa bongo,
hatimaye akajikuta akiogelea umaarufu.
5.Chaga Barbie
Huyu
alijipatia umaarufu baada ya kujihusisha kimapenzi na msanii wa Kenya
Prezzo, jina lake lilivuma zaidi pale walipozinguana na Prezoo hadi
kufikia hatua ya kutoleana maneno mbofu mbofu mitandaoni. Ni kati ya
watu wanaofuatiliwa sana mitandaoni.
6.Petit man wakuache
Huyu
jamaa amefahamika kupitia Wema Sepetu, jina lake limevuma na kutajwa
tajwa sana baada ya kuwa karibu na madame. Sio muigizaji wala
mwanamuziki.
7.Najma
Huyu
ni ex wa Mr blue, nae alianza kufahamika baada ya kujiingiza kwenye
mahusiano na msanii huyo. Scandal yake ya kutoka na Diamond ilimuongezea
credit kwa kiasi flan na kumfanya aongelew sana mitandaon, alishawah
kujarib mziki pia na filamu.
8.Clement
Picha yake haijapatikana mpaka leo |
huyu
alifahamika baada ya kujiingiza kwenye mahusiano na super star Wema
Sepetu, ni kati ya watu wanaozungumzwa sana mitandaoni hadi kesho,
japokuwa sura yake haifahamiki kihivyo, bado watu wanapenda kujua kuhusu
yeye na maisha yake.
9.Ostadh Juma
Watu
mjini wanatafuta umaarufu kwa kasi, baada ya kuzipata pesa kwa wingi ,
aliamua Ku manage wasanii kama PNC, dogo Janja na wengine japokuwa hana
management skills nzuri. Kumrudisha dogo Janja dar es salaam na kumweka
kwenye kundi lake la watanashati entertainment pamoja na kumpiga picha
PNC alipokuwa akijaribu kumuomba msamaha kumemfanya aongelewe zaidi na
kufuatiliwa maisha yake mbaya zaidi hadi ya wazazi wake kitu ambacho
kimem cost kwa kiasi Fulani.
10. Kajala Masanja
Kwenye
mtandao wa instagram ana followers karibia elfu thelathini na kitu,
wote wametokana na promo ya maana kwa shoga yake Wema Sepetu, kutolewa
rumande na Wema Sepetu kumemuongezea umaarufu zaidi na kuwa miongoni mwa
watu wanaozungumzwa sana, jina la kajala limekaa sana mdomoni mwa Wema
Sepetu, hivyo kumfanya apate mashabiki wengi zaidi kupitia Wema. Ni
mcheza filamu za kibongo.
No comments:
Post a Comment