Pages

Sunday, May 4, 2014

CHELSEA YALAZIMISHWA SARE NA NORWICH CITY YA 0-0 LIGI KUU UINGEREZA LEO


 Gary CahillJohan Elmander Chelsea Norwich City Premier League 05042014
Kweli kazi ipo...mpira katika harakati za kugombewa ambapo Chelsea na Norwich City leo ziliweza kugawana point baada ya kutoka 0-0

Timu ya Chelsea ya Uingereza leo imepoteza matumaini ya kuutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya kulazimishwa sare na timu ya Norwich city iliyopigwa leo kwenye uwanja wa Stamford Bridge. 
   Chelsea ilitabiriwa mapema kuwa ingeweza kupata magoli ya kutosha leo kutokana na kuifukuzia kwa hali na mali ubigwa wa Uingereza. Dhahiri shahiri inaonyesha Ubingwa sasa unagombewa na Man city na Liverpool pekee.
Kwa matokeo hayo Chelsea itabakia katika nafasi yake ya tatu nyuma ya Liverpool ambapo ligi sasa inaongozwa na Manchester City ikilingana points na Liverpool lakini Man City ikiongoza kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Chelsea v Norwich City: live
Nemanja Matic (kushoto) na Jonny Howson wakiwa katika harakati za kugombea mpira. Chelsea na Norwich City walitoka sare ya bila kufungana kwenye mechi yao ya leo.

No comments:

Post a Comment