Kampuni tano zimepanda dau la kutaka kununua leseni za kutafuta mafuta na gesi katika himaya ya Tanzania.
Hata hivyo idadi hiyo ni ndogo zaidi kuliko vitalu vinane vilivyokuwa vikinadiwa katika duru hii, TPDC imeeleza.
Tanzania, ambayo imegundua kiasi kikubwa cha
gesi ya asili katika mikoa ya kusini, ilitangaza vitalu saba vya maji
marefu baharini na kimoja katika Ziwa Tanganyika.
Kampuni ya CNOOC Ltd na Gazprom
inayoendeshwa na serikali ya Urusi ni miongoni mwa makampuni makubwa ya
kigeni yaliyowasilisha maombi yao katika mzunguko huo wa nne.
Miamba mingine ya nishati Statoil na
ExxonMobil, ambayo imegundua kiasi kikubwa cha gesi Tanzania,
iliwasilisha maombi ya pamoja kupata kitalu kimoja.
“Mchakato wa kutathmini utaanza mara moja na
tutatangaza washindi wa mnada haraka iwezekanavyo kadri muundo wa
ushughulikiaji wa leseni unavyoruhusu,” Yona Killagane, mkurugenzi
mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) aliieleza Reuters.
Killagane hakusema lini washindi watatangazwa. Muda wa mwisho kuwasilisha maombi ilikuwa Mei 15.
No comments:
Post a Comment