Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Mgambo kitongoji cha Lukula kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkani
Tabora ambapo aliwaomba radhi wakulima wa Tumbaku kwa kadhia waliyo nayo
kutokana na kunyonywa na kutopata haki zao za malipo kwa miaka 3.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la
Sikonge Said Mkumba wakiwasomea wananchi wa kijiji cha Lukula maeneo
yatakayopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Sikonge.
Mbunge
wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba akihutubia wananchi wa kijiji cha
Lukula kata ya Mgambo na kuwaambia wale wote waliodhulumu wakulima
wanatakiwa kuchukuliwa hatua na pia alisisitiza sheria zingatiwe za
wanasiasa kutojihusisha na masuala ya vyama vya ushirika.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa mbali mbali kabla
ya kuhutubia wakazi wa kata ya Mgambo,Katibu Mkuu wa CCM amehuzunishwa
sana na baadhi ya viongozi wa Serikali kutofika kwa wananchi na kujua
matatizo yao badala yake wamesababisha wananchi kuumia sana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa jengo
la upasuaji na Dk.Silvanus Kabutura Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya
cha Kata ya Kitunda wilayani Sikonge,Daktari Kabutura alimueleza Katibu
Mkuu wa CCM changamoto kubwa uhaba wa maji katika kituo hicho.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua jengo la upasuaji
la kituo cha afya cha Kitunda wilayani Sikonge mkoani Tabora ambalo
limechelewa kukamilika kwa zaidi ya mwaka mmoja na huku Wizara ya Afya
kushindwa kuchukua hatua mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment