Pages

Sunday, June 1, 2014

KINANA LEO ZIARANI WILAYA YA SIMANJIRO BAADA YA KUMALIZA NA WILAYA YA KITETO


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Siasa wilaya ya Kiteto na mkoa wa Manyara,katika kikao kilichofanyoka kwenye ukumbi wa CCM wilaya.
Wananchi jamii ya Kimasai wakiwa na bango lao wakisubiri kuwasiri kwa msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Kimotorok wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wananchi jamii ya Kimasai katika Kijiji cha Kimotorok baada kumsimamisha na kumuelezea changamoto walizonazo,hasa mgogolo mkubwa wa ardhi kati yao na hifadhi.
Kinana akisalimiana na wananchi jamii ya Kimasai mara baada ya kuzungumza nao katika kijiji cha Kimotorok,wilayani Kiteto mkoani Manyara,ambako inaelezwa kuwa kuna mgogolo mkubwa wa ardhi,kati ya Wafugaji na wakulima,wafugaji na hifadhi,Kinana ameahidi kuyasikiliza matatizo hayo na kueleza kuwa atayafikisha katika ngazi ya juu na kuhakikisha ufumbuzi wa kina unafanyika na kupatikana kwa wakati.
Kinana akisalimiana na wazee wa kimila wa Kimasai
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitazama sehemu maalum ya kunyweshea maji mifugo,ambayo yeye mwenyewe aliiizindua
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama wa jamii ya kimasai,mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama wenye thamani ya shilingi bilioni mbili na zaidi katika kijiji cha Ilela kata ya Esekii wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia waanchi wa kijiji cha Nalangton,Wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Baadhi ya Vijana wa Boda boda akiwa na bango lao
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipanda mti kwenye moja ya shule ya msingi ya Laalakir,ilioko mjini Kibaya,Wilayani Kiteto,shule ya Wakulina na Wafugaji ambayo imekuwa ikifanya vizuri wilayani humo,mkoani Manyara.
Sehemu ya Umati wa wananchi wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kiteto,Mh.Benedict Ole Nangoro katika kijiji cha  cha Irkiushbor,wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi mara baada ya kupokelewa katika kijiji cha Irkiushbor,wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 200 na zaidi,katika  kijiji cha Ilela kata ya Esekii wilayani Kiteto mkoani Manyara. 

No comments:

Post a Comment