Pages

Wednesday, May 28, 2014

LEO NI MWAKA MMOJA TOKA AFARIKI NGWEA

Marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’
STAA wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ leo anatarajiwa kufanyiwa shughuli ya kumbukumbu ya kifo chake. Habari kutoka ndani ya familia ya Ngwea zinasema kuwa, shughuli hiyo itafanyika leo Mei 28, nyumbani kwao Morogoro ikiwa ni mwaka mmoja timilifu tangu afariki dunia.
Ngwea alifariki dunia Mei 28, mwaka jana katika Hospitali ya St. Hellen jijini Johannesburg, Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment