Liverpool wameona giza huku kombe la Ligi ya Premier likiwakwepa baada ya kwenda sare ya mabao matatu dhidi ya Crysral Palace .
Cha kushangaza ni kwamba Liverpool walikuwa
mbele kwa mabao matatu lakini Cyrstal walitifua kivumbi na kutoka nyuma
bila bao huku wakimaliza mechi kwa mabao matatu sawa na Liverpool.Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez waliiweka mbele klabu yao katika muda wa saa moja kwa mabao matatu.
Steven Gerrad akiwa haamini kilichotokea baada ya mpira kuisha
Hali hii iliwachaa mashabiki wa Liverpool vinywa wazi wasijuie cha kusema.
Liverpool sasa wako mbele ya Man City kwa poiti moja tu kwenye jedwali la alama.City bado wako na mechi moja kucheza.
City watamenyana na Aston Villa katika uwanja wa Etihad mnamo siku ya Jumatano, kabla ya kumaliza msimu kwa mechi nyingine dhidi ya West Ham Jumapili.
No comments:
Post a Comment