Pages

Saturday, May 17, 2014

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI KATIKA MKUTANO WA UKAWA MJINI IRINGA



Profesa Ibrahim Lipumba akikaribishwa na Mchungaji Peter Msigwa (mbunge wa Iringa Mjini )kuhutubia mamia ya wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza


Huu ndio ulikuwa muitikio wao, wakisisitiza serikali tatu kama walivyotoa maoni yao kwa Tume ya Katiba

Mchungaji Msigwa akiamsha hali kwa wananchi hao

Profesa Lipumba akionesha rasimu iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kujadiliwa na bunge maalumu la katiba

Danda Juu wa NCCR-Mageuzi alikuwepo pia na akazungumza machache anayofahamu kuhusu rasimu hiyo, msisitizo ukiwa ni serikali tatu kama ilivyopendekezwa na katika rasimu


Sheikh Rajab Katimba wa Shura ya Imam alikuwepo na kuzungumzia umuhimu wa bunge la katiba kujadili maoni ya wananchi. Alisisitiza umuhimu wa kuwa na serikali ya Tanganyika kama ilivyo visiwani  ambako Zanzibar wana serikali yao

Diwani wa kata ya mivinjeni Iringa Mjini, Frank Nyalusi alikuwepo na akarusha lawama kwa jeshi la Polisi kwa kutisha watu ili wasipate katiba wanayotaka

Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa, Allein alikuwa mshehereshaji wa mkutano huo wa Ukawa

Moja ya mabango yaliyopamba mkutano huo na ujumbe wake kama unavyosomeka

No comments:

Post a Comment