Pages

Friday, May 30, 2014

PROF. MUHONGO AWASILISHA BUNGENI BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

      Waziri wa Nishati na MadiniProfesa Sospeter Muhongo akiwa anawasilisha hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati na madini ya mwaka 2014/15 leo mjini Dodoma.  

   DONDOO CHACHE KATIKA HOTUBA HIYO

UKUAJI WA SEKTA YA NISHATI
  Dira ya Maendeleo ya Taifa (Tanzania Development Vision, 2025) ilianza kutekelezwa Mwaka 2000. Kupitia Dira hiyo, Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imedhamiria kujenga uchumi wa kisasa utakaoiwezesha Tanzania kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja (GDP per capita) kutoka wastani wa Dola za Marekani 640 hadi 3,000 ifikapo Mwaka 2025. Ili kufikia lengo hilo, nchi inahitaji kuwa na nishati ya kutosha, yenye uhakika na ya gharama nafuu. Kwa kutambua hilo, Serikali imeendeleza jitihada za kuboresha upatikanaji wa nishati bora vijijini na mijini kwa kuongeza uwekezaji katika miundombinu ya nishati ikiwemo ya umeme, gesi asilia na mafuta. 

GESI ASILIA NA MAFUTA 
  Hadi kufikia Mwezi Aprili, 2014 mabomba yote 45,693 kwa ajili ya ujenzi wa Bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Mtwara (Madimba) na Lindi (Songo Songo) hadi Dar es Salaam yalikuwa yameletwa nchini. Ufukiaji wa mabomba hayo umekamilika kwa umbali wa kilomita 182 kati ya 542 sawa na asilimia 34. Kazi ya ujenzi wa Bomba la kutoka Songo Songo kupitia baharini hadi Somanga Fungu, lenye urefu wa kilometa 25.6 imekamilika kwa asilimia 100. Kwa ujumla ujenzi wa Bomba la gesi asilia umekamilika kwa asilimia 78. Kazi ya kuweka mkongo wa mawasiliano (Fibre Optic Cable) inafanyika sambamba na ufukiaji wa Bomba. Aidha, mtambo wa kuchimbia mabomba (horizontal drilling) katika Mto Rufiji uliletwa nchini Mwezi Aprili, 2014. shughuli za ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi asilia katika eneo la Madimba, Mtwara na Songo Songo, Lindi zinaendelea. 
    Hadi kufikia Mwezi Aprili, 2014 ujenzi wa nyumba za kuishi wafanyakazi kwaeneo la Madimba ulikuwa 38umekamilika kwa asilimia 90 na Songo Songo kwa asilimia 78. Aidha, ujenzi wa misingi (foundations) ambako mitambo ya kusafisha gesi asilia itafungwa umekamilika. Vilevile, utengenezaji (manufacturing) wa mitambo yote ya kusafisha gesi asilia umekamilika kwa asilimia 60.Mitambo hiyo itaanza kuwasili nchini kuanzia Mwezi Julai, 2014 kutoka Jamhuri ya Watu wa China. Kwa ujumla maandalizi ya kufunga mitambo ya kusafisha gesi asilia yamekamilika kwa asilimia 45. 
   Serikali imedhamiriakwa dhati kukamilisha ujenzi wa Bomba ifikapo Mwezi Julai, 2014 na mitambo ya kusafisha gesi asilia ifikapo Mwezi Desemba, 2014. Mradi huu utagharimu Dola za Marekani bilioni 1.2, sawa na takriban Shilingi trilioni 2. Fedha za ndani zilizotengwa kwa Mwaka 2014/15 ni Shilingi bilioni 148.Katika Mwaka 2013/14, jumla ya futi za ujazo trilioni 4.8 za gesi asilia ziligunduliwa katika visima vya Mkizi – I, Ngisi – I, Tangawizi – I, na Mlonge – I. 
    Hadi kufikia Mwezi Aprili 2014, kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa nchini ni futi za ujazo trilioni 46.5, sawa na mapipa ya mafuta bilioni 8.37. Kiasi hiki ni takriban mara tano ya gesi asilia iliyokuwepo Mwaka 2005 wakati Serikali ya Awamu 42 ya Nne inaingia madarakani. Kati ya kiasi hicho, asilimia 83 ni kutoka kina kirefu cha maji Baharini na asilimia 17 ni nchi kavu. 

MAUZO NA THAMANI YA MADINI YALIYOUZWA NJE YA NCHI
    Katika Mwaka 2013/14 Wizara iliendelea kusimamia shughuli za utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini kwa lengo la kuongeza mchango wa Sekta hii kwenye Pato la Taifa. Kutokana na mipango na miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na Serikali, Sekta ya Madini imeendelea kuwa chachu katika ukuaji wa uchumi nchini. Hata hivyo, Sekta ya Madini ni mojawapo ya sekta zilizoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mtikisiko wa uchumi Duniani ambao uliambatana na kushuka kwa bei ya madini mbalimbali, hususan dhahabu na pia kushuka kwa upatikanaji wa mitaji ya nje (FDI).
   Thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi yaliyouzwa na Migodi Mikubwa ya Dhahabu iliongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 640 Mwaka 2005 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 1.79 Mwaka 2013. Uzalishaji wa madini ulipungua kutoka wakia 1,398,406 Mwaka 2005 hadi wakia 1,244,743 Mwaka 2013, sawa na punguzo la asilimia10.9. Aidha, asilimia 69.27 ya mauzo ya madini yote ya migodi mikubwa nje ya nchi kwa Mwaka 2013 ilitokana na mauzo ya dhahabu. Kwa upande wa uzalishaji na mauzo ya madini katika migodi mikubwa nchini katika kipindi cha Mwaka 2013, jumla ya wakia milioni 1.24 za dhahabu, wakia 380,000 za fedha na ratili milioni 17.70 za shaba zilizalishwa na kusafirishwa nje ya nchi kutoka migodi mikubwa ya Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, Golden Pride, New Luika, North Mara na Tulawaka. Jumla ya thamani ya madini hayo ni Dola za Marekani bilioni 1.79 pungufu kwa asilimia 17.7 ukilinganisha na mauzo ya madini yaliyofanywa na migodi hiyo kwa Mwaka 2012 ya Dola za Marekani bilioni 2.17. Vilevile, jumla ya karati 158,562 za almasi na gramu milioni 3.24 za Tanzanite zilizalishwa na migodi ya Mwadui na TanzaniteOne, sawia. Mauzo yote ya almasi na Tanzanite yaliyofanywa na migodi hiyo kwa Mwaka 2013 yalifikia Dola za Marekani milioni 50.53. Mrabaha uliolipwa Serikalini na wamiliki wote wa migodi mikubwa nchini katika kipindi hicho ni Dola za Marekani milioni 72.90, sawa na Shilingi bilioni 116.64. Mgodi wa Tulawaka uliopo Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera ulifungwa rasmi Mwezi Julai, 2013. Aidha, mgodi wa Golden Pride uliopo Wilaya ya Nzega, Mkoa wa Tabora ulifungwa rasmi Mwezi Februari, 2014. Ni wazi kuwa, kufungwa kwa migodi hiyo kutapunguza uzalishaji wa dhahabu na mapato ya Serikali.

MAOMBI YA FEDHA
Wizara inaomba fedha Jumla ya Shilingi 1,8,255,652,000 za kitanzania.

No comments:

Post a Comment