Pages

Saturday, April 12, 2014

MVUA YA LEO NI DAR MPAKA MORO YAENDELEA KUWATESA WANANCHI, MOROGORO NAKO HAKUFAI

 Baadhi ya Nyumba zikiwa zimezungukwa na maji katika Eneo la Mzambarauni Mkoa wa Morogoro kutokana na Mvua zilizo nyesha.
 
Huyu jamaa anasubiri manusura.....hapo jijini Dar
 Maji ya mvua yaliyosababisha mafuriko yakipita kwa kasi katika daraja la Mzambarauni mjini Morogoro.
 
Hapa ni eneo la Msasani jijini Dar....jamaa wakijaribu kuokoa baadhi ya mali zao walizofanikiwa kuwahi.
 Nyumba zikiwa zimezungukwa na maji....
 
Jamaa akiduwaa asijue la kufanya....
 Mtoto huyu akijitahidi kupunguza maji yaliyojaa ndani kwao kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha na kusababisha mafuliko Mkoa wa Morogoro.
 Wakazi wa Morogoro wakipita ndani ya maji kutokana na Mvua kubwa iliyosababisha mafuliko leo.
 Nyumba iliyokuwa ikiendelea kujengwa ikiwa imeezuliwa na upepo huku ikiwa imezungukwa na maji.
 Hatari tupu hapa hata wasafiri hawakuweza tena kuingia eneo hili kupata chochote kutokana na eneo hili kujaa maji.
Wakazi wa Morogoro wakiangalia baadhi ya nyumba zilizoezuliwa na upepo na kuzingirwa na maji.

No comments:

Post a Comment