Rais wa malawi Joyce Banda, ametangaza rasmi kusitisha na kuyafuta matokeo ya Uchaguzi uliofanyika nchini kwake kuanzia jumanne ya wiki iliyopita, baada ya Tume ya uchaguzi kuanza kutoa matokeo ya uchaguzi huo ambayo hadi sasa asilimia 30 ya kura hizo inaonyesha Mgombea wa Chama cha upinzani cha Democratic Progressive Party-DP Prof. Peter Mutharika, anaongoza akiwa na jumla ya kura 683, 621.
Anayefuatia kwa kura ni Rais Joyce Banda, wa Peoples Part akiwa na kura 372, 101.
Anayeshika
nafasi ya tatu katika uchaguzi huo ni Mchungaji Dkt. Lazarus Chakwera,
wa Chama cha DPP, akiwa na kura 289, 145, na nayefuatia ni Atupele
Muluzi wa Chama cha United Democratic Front-UDF akiwa na kura 269,250.
No comments:
Post a Comment