Rais Kikwete akiwa na Samatta kulia na Ulimwengu kushoto mjini Kinshasa |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana
amewatembelea washambuliaji wawili Watanzania wanaocheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Ally Samatta na Thomas Emannuel Ulimwengu.
Tovuti
ya TPM imeandika kwamba Rais Kikwete aliwatembelea wachezaji hao leo
mjini Kinshasa ambako wapo na timu yao kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu
ya DRC dhidi ya mahasimu wao katika mbio za ubingwa AS Vita.
Rais Kikwete aliye ziarani DRC, alikuwa ameambatana na maofisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania majira ya Saa 6:15 mchana alipokutana na wachezaji hao pamoja na Mwenyekiti wa klabu yao, Moses Katumbi.
Rais
Kikwete yupo Kinshasa tangu jana usiku kwa ziara maalum ya Saa 24 juu
ya ushirikiano wa DRC na Tanzania, ambako alikutana na rais mwenzake wa
huko, Joseph Kabila.
Kikwete
alitumia robo saa kuzungumza na akina Samatta katika hoteli ya Congo
River, ambako wameweka kambi kwa ajili ya mechi ya kukata na shoka
kesho.
Rais
Kikwete aliwakumbusha Samatta na Ulimwengu kwamba, Watanzania
wanajivunia kuwaona wakiwa na jezi za TPM na kwamba wao ni tegemeo la
timu ya taifa, Taifa Stars kwa sasa.
No comments:
Post a Comment