Rais Dkt. Jakaya Kikwete akipokelewa na mfanyabiashara na muwekezaji mkubwa na maarufu nchini Nigeria Alhaji Aliko Dangote katika kiwanja cha ndege cha kiwanda chake cha cement cha Dangote Cement Obajan Plant kilichopo kilomita 400 kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembelea mnamo tarehe 9 May 2014 na kushoto ni balozi wa Nigeria nchini Tanzania mh. Dkt Ishaya Samalia Majanbu.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mfanyabiashara na mwekezaji Maarufu nchini Nigeria Alhaji Aliko Dangote,wakati alipokuwa akizungushwa katika kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kinachomilikiwa na mwekezaji huyo tarehe 9 May 2014
Rais Kikwete akitembezwa katika kiwanda cha saruji huku akipata maelezo kutoka kwa wataalamu kutoka katika kiwanda hicho cha Dangote Cement Obajan Plant kinachomilikiwa na mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote wa Nigeria.
Rais Kikwete akitembezwa na Alhaji Aliko Dangote katika sehemu mbalimbali za kiwanda cha saruji kujionea shughuli zinavyofanyika katika kiwanda hicho jana tarehe 9 May 2014.
Rais Kikwete akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam wa kiwanda cha Saruji cha Dangote Cement Obajan Plant alipotembelea jana kilomita 400 kaskazini mashariki mwa Lagos.
Rais Kikwete akionyeshwa Malighafi zinazotumika kenye kiwanda cha Saruji cha Dangote Cement Obajan Plant alichokitembelea jana.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitia saini mfuko wa Saruji alipotembelea kiwanda cha Saruji cha Dangote Cement Obajan Plant jana.
No comments:
Post a Comment