JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na
uvumba Emmanuel Mbasha (kulia pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa
nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake
mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu
makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu
iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na.
TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014
akidai kufanyiwa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili) wiki
iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho
sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo
ndani ya gari lake hali ambayo ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa
Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.
Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu makali aliyoyapata
mlalamikaji huyo ilibidi aende Hospitali ya Amana na kugundulika
kuwa aliingiliwa kimapenzi na kumsababishia michubuko sehemu za
siri.
HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha waliozaliwa jijini Mwanza na mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa
muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua
kumtoa mtoto mmoja kwa mama mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea,
wakati huo mtoto huyo alikuwa na miezi mitatu.
Ikaelezwa kuwa, mama wa Flora alikaa na mtoto huyo akimsomesha hadi
alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye
hadi alipofikwa na janga hilo.
Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza kufanya kitendo hicho kwa
sababu mkewe (Flora) ameondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa
kile kilichodaiwa kwamba kuna ugomvi mkubwa ndani ya ndoa yao.
Taarifa zaidi zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo nyumbani kwake huku
mlalamikaji yuko Hospitali ya Amana akiendelea kufanyiwa uchunguzi
wa kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la!
Kwa upande wake mlalamikaji huyo alipopigiwa simu juzi kwa lengo
la kuthibitisha kuhusiana na sakata hilo alikiri na kusema
amekwishatoa taarifa polisi kwa kitendo alichofanyiwa na mwenye
nyumba huyo huyo.
No comments:
Post a Comment