Waangalizi 7 wa kimataifa
waliokamatwa siku nane zilizopita na wanaharakati wanaounga mkono
Urusi,wamewachiliwa huru,pamoja raia watano wa Ukraine waliokuwa nao.
Kiongozi wa kundi la raia wa Ukraine wanaotaka
kujitenga na taifa hilo mjini Sloviansk Vyacheslav Ponomaryov ,ameelezea
kwamba waangalizi hao ni wageni wake na kwamba wamewachiliwa bila
vikwazo.Urusi imekuwa chini ya shinikizo ya mataifa ya magharibi kuwaachilia huru waangalizi hao ili kupunguza hali ya wasiwasi mashariki mwa Ukraine.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo amesema kuwa waangalizi hao waliweza kuachiliwa huru kupitia mjumbe mmoja wa Urusi Vladmir Lukin.
No comments:
Post a Comment