Juhudi za uokoji zinaendelea
siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao
elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika
maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa
wa karibu mita kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja
kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.Miili ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana makazi.
Mashirika ya misaada na uokoaji kwa sasa wameanza kuwapa mikate na maji maelfu ya watu waliolala nje kwenye baridi kali wakiwa hawana makazi.
"Taarifa zinasema ardhi na matope yameendelea kuporomoka ambapo wengi ya waliokufa ni waokoaji ambao walikwenda kutoa msaada kwa wenzao."
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo.
No comments:
Post a Comment